Return to Video

Hotuba ya Steve Jobs kwenye Sherehe ya Mahafali, Chuo Kikuu cha Stanford Mwaka wa 2005

  • 0:06 - 0:08
    [Chuo Kikuu cha Stanford www.stanford.edu]
  • 0:08 - 0:13
    Mtangazaji: Kipindi hiki kimewaletea na Chuo Kikuu cha Stanford. Tafadhali wasiliana nasi kwa stanford.edu
  • 0:15 - 0:22
    [upigaji makofi]
  • 0:22 - 0:23
    Steve Jobs: Asanteni
  • 0:25 - 0:27
    [Steve Jobs - Mkurugenzi Mkuu Apple na Pixar Animation]
  • 0:27 - 0:32
    Ni heshima kwangu kuwepo na nyinyi katika sherehe ya mahafali ya kutunuku shahada kutoka katika chuo kikuu ambacho ni kimojawapo bora katika dunia nzima.
  • 0:32 - 0:35
    [ukelele wa kufurahia]
  • 0:36 - 0:46
    Kusema kweli mimi sijatunukiwa shahada ya chuo kikuu na hii ni mara yangu ya kwanza kuhudhuria mahafali yoyote.
  • 0:46 - 0:48
    [vicheko]
  • 0:48 - 0:54
    Leo naomba niwasimulie visa vitatu vilivyotokea maishani mwangu. Vitatu tu, basi.
  • 0:55 - 0:59
    Cha kwanza ni juu ya kuunganisha nukta.
  • 1:01 - 1:08
    Niliacha masomo katika Chuo cha Reed baada ya muda wa miezi sita za kwanza katika mwaka wa kwanza, halafu nikakaa kama mgeni kwa muda wa miezi kumi na nane hivi kabla ya kusimamisha masomo kabisa.
  • 1:09 - 1:11
    Kwa nini niliacha masomo?
  • 1:12 - 1:14
    Sababu inatangulia kuzaliwa kwangu.
  • 1:15 - 1:21
    Mama mzazi yangu alikuwa msichana hajaolewa alikuwa akitimiza shahada ya uzamili akaamua niwe mtoto wa kupanga.
  • 1:22 - 1:26
    Alikuwa na msimamo wa dhati nilelewe na watu waliotimiza shahada ya chuo kikuu.
  • 1:26 - 1:31
    Kwa hivyo mpango ukafanyika niasiliwe na mwanasheria na mkewe.
  • 1:32 - 1:37
    Isipokuwa nilipoibuka mtoto wa kiume dakika la mwisho wakaamua wanataka mtoto wa kike.
  • 1:38 - 1:42
    Kwa hivyo wazazi wangu walioandikwa katika orodha ya wanaosubiri kumwasili mtoto walipigiwa simu usiku wa manane na wakaulizwa:
  • 1:43 - 1:49
    "Tumepata mtoto wa kiume asiyetarajiwa; mnamtaka?"
    Wakajibu: "Bila shaka."
  • 1:51 - 1:58
    Baadaye mama mzazi yangu aligundua mama yangu alikuwa hajamaliza chuo kikuu huku mumewe baba yangu hajamaliza shule ya sekondari.
  • 1:59 - 2:02
    Akakataa kutia sahihi hati maalum ya kuasiliwa.
  • 2:03 - 2:12
    Baada ya miezi michache kupita akakubali shingo upande kutokana na ahadi ya wazazi wapya ya kuwa mimi nitasoma chuo kikuu. Hayo ndiyo yalikuwa mwanzo wa maisha yangu.
  • 2:14 - 2:21
    Baada ya miaka kumi na saba kupita nilianza chuo kikuu lakini katika ushamba wangu nikachagua chuo ghali karibu sawa na Stanford.
  • 2:22 - 2:27
    Pesa zote za akiba ya wazazi wangu tabaka yao ya wafanya kazi, zilitumika kulipia ada zangu za chuo kikuu.
  • 2:27 - 2:30
    Baada ya muda wa miezi sita sikuona thamani ya masomo hayo.
  • 2:30 - 2:36
    Sikuwa na mpango wa maisha mbali na uwezo wa chuo kunisaidia katika kufafanua mpango upi unanifaa zaidi.
  • 2:37 - 2:41
    Huku nikitumia pesa zote za akiba ya maisha ya wazazi wangu.
  • 2:42 - 2:47
    Basi nikakata shauri kuachana na masomo nikiamini mambo yatakuwa shwari.
  • 2:47 - 2:52
    Wasiwasi ilinikumba wakati huohuo lakini sasa nikilitafakari shauri hilo ni miongoni mwa yale bora katika maisha yangu.
  • 2:53 - 2:54
    [vicheko]
  • 2:54 - 2:59
    Pindi tu nilipoachana sikulazimishwa kuchukua madarasa yale ambayo hayakunivutia.
  • 3:00 - 3:04
    Nikaenda kwa yale yaliyovutia kwangu.
  • 3:05 - 3:14
    Sikuwa na maisha ya starehe. Sikuwa na chumba katika bweni. Ilibidi nilale sakafuni katika vyumba vya marafiki. Nilikuwa nikiokota chupa kupata senti za kununulia chakula.
  • 3:14 - 3:21
    Kila Jumapili mimi hutembeza maili saba ili nipata lishe maalum katika hekalu ya Wahindi wafuasi wa dini ya Hare Krishna.
  • 3:22 - 3:23
    Niliipenda mno.
  • 3:24 - 3:30
    Mengi niliyowahi kutokana na upekuzi wangu pamoja na uwezo wangu kuelewa yakawa adimu nyakati za baadaye.
  • 3:30 - 3:31
    Hebu, nitoe mfano mmoja:
  • 3:33 - 3:38
    Wakati huo Chuo cha Reed kilikuwa na ufundisho bora wa utaalamu wa maandiko kuliko vyuo vyote vingine nchini.
  • 3:38 - 3:45
    Kwenye eneo la chuo kila tangazo, kila kitambulisho kwenye mitoto ya meza kilichorwa vizuri sana.
  • 3:45 - 3:52
    Kwa sababu nimeshajitoa masomoni sikulazimishwa kuchukua madarasa yanayotakiwa na nikaamua kuchukua darasa la utaalamu wa maandiko nijifunze jinsi ya kufanya.
  • 3:53 - 3:59
    Nilijifunza aina za chapa mifano ni serif na sans serif, juu ya upimaji nafasi katikati ya michanganyiko tofauti ya herufi,
  • 4:00 - 4:02
    na juu ya ukamilifu wa utaalamu wa maandiko, kitu gani kinaleta ukamilifu.
  • 4:03 - 4:11
    Kujifunza huko kulikuwa kuzuri, kwenye usanaa usio na kujivuna mbali na mazingira ya kisayansi, kwangu mimi nilivutiwa kupindukia.
  • 4:12 - 4:16
    Sikuwa na matumaini ya kuyatumia masomo hayo katika kazi nitakayofanya,
  • 4:17 - 4:23
    Lakini baada ya muda wa miaka kumi kupita tulipokuwa tunabunia tarakilishi ya kwanza aina ya Mactintosh nikafikiria upya mafundisho hayo.
  • 4:23 - 4:29
    Tulitumia kabisa katika ubunaji wa Mac ambayo ilikuwa tarakilishi ya kwanza kuwa na utaalamu mzuri wa maandiko.
  • 4:29 - 4:32
    Nisingeli kuwa mgeni katika darasa hilo nilipokuwa ninahangaika kwenye chuo,
  • 4:32 - 4:37
    tarakilishi iitwayo Mac haikungali kuwa na aina nyingi za herufi wala herufi zenye uwiano wa nafasi za katikati zao.
  • 4:37 - 4:42
    Na kwa sababu Windows iliiga Mac haielekei tarakilishi za kibinafisi zozote zingekuwa nazo kamwe.
  • 4:42 - 4:49
    [vicheko na upigaji makofi]
  • 4:50 - 4:54
    Nisipongeliachana na masomo singalipitia darasa lile la utaalamu wa maandiko.
  • 4:54 - 4:58
    matokeo yake tarakilishi ya kibinafsi hazingekuwa na vivutio kiasi zinazokuwa nazo.
  • 4:58 - 5:02
    Bila shaka ilikuwa haiwezekani kuunganisha nukta zitakazokuja mambo ya usoni nilipokuwa chuoni.
  • 5:02 - 5:06
    Lakini mambo yakadhihirika kweupe nikirudia nyuma baada ya muda wa miaka kumi kupita.
  • 5:07 - 5:12
    Kutia mkazo kauli hiyo, huwezi kuunganisha nukta za mambo ya usoni; ni zile tu zilizokwisha fanyika ambazo zinaweza kuzingatiwa ziunganishwe,
  • 5:12 - 5:16
    Lazima uamini nukta za baadaye zitaunganika katika maisha yako ya baadaye.
  • 5:16 - 5:21
    Sharti uwe na uaminifu wa huenda moyo wako, majaliwa, maisha, hulka zako, na kadhalika.
  • 5:21 - 5:27
    Kwa sababu kuamini nukta zitaunganika baadaye kutakutilia moyo na imani kupiga njia uliyoinyoshea wewe mwenyewe.
  • 5:27 - 5:32
    Hata ukifuata njia isiyo ya kawaida, uaminifu ndio utakunyoshea.
  • 5:38 - 5:42
    Kisa changu cha pili ni juu ya upendo na kukosa upendo.
  • 5:43 - 5:48
    Mimi nilibahatika - nilipata kujua ninavyopenda kufanya nikiwa bado mvulana.
  • 5:48 - 5:51
    Mimi pamoja na rafiki yangu jina lake Woz tulianzisha kampuni la Apple kwenye kibanda cha gari nyumbani kwao wazazi wangu na mimi nikiwa na umri wa miaka ishirini.
  • 5:51 - 5:59
    Tulifanya kazi kwa bidii na baada ya muda wa miaka kumi kampuni ya Apple iliyoanzia na watu wawili sisi tukiwa kwenye kibanda, ilikua kupata thamani ya dola bilioni mbili ikiwa na waajiriwa zaidi ya elfu nne.
  • 6:00 - 6:05
    Tulikuwa tumetoa maumbile yetu bora - Macintosh, mwaka mmoja kabla, nami nikipata umri wa miaka thelathini.
  • 6:06 - 6:07
    Kisha nikafukuzwa kazini.
  • 6:09 - 6:11
    Je, inawezaje kufukuzwa kutoka kampuni uliyoanzisha wewe mwenyewe?
  • 6:12 - 6:18
    Basi kama kampuni ya Apple ilivyoendelea kukua tukaajiri mtu mwenye kipaji kizuri kuongoza kampuni akiwa na mimi,
  • 6:18 - 6:21
    na mwaka wa kwanza mambo yakawa shwari.
  • 6:21 - 6:25
    Halafu baada ya hapo mitazamo yetu ikaanza kutengana hatimaye tukafarakana.
  • 6:25 - 6:28
    Tulipofarakana baraza letu la wakurugenzi wakamuunga mkono yeye.
  • 6:28 - 6:32
    Kwa hivyo nikiwa na umri wa miaka thelathini nilifukuzwa kazi bayana ikatangazwa kwenye magazeti.
  • 6:33 - 6:37
    Kitu kilichokuwa kitovu cha maisha yangu nikiwa mtu mzima kimekwisha, nami nikadhoofika.
  • 6:38 - 6:40
    Kwa muda wa miezi michache, kweli nilikuwa sikujua la kufanya.
  • 6:41 - 6:47
    Niliona nimewasikitisha wale wajasiriamali wa kizazi kilichotangulia - nikashindwa kubeba amali ilyonipasa niibebe.
  • 6:48 - 6:53
    Tulikutana na David Packard pamoja na Bob Noyce nikaomba radhi kwa kuharibu mambo.
  • 6:54 - 6:58
    Kushindwa kwangu kulijulikana na wengi hata nilifikiri kukimbia Bonde.
  • 6:58 - 7:03
    Lakini katika mwendo polepole nilitanabahi ya kuwa bado niliipenda kazi yangu.
  • 7:04 - 7:11
    Mambo yaleyale ya mabadiliko pale Apple hayajaubadilisha upendo wangu hata kidogo.
  • 7:12 - 7:13
    Kwa hivyo basi nikaamua kuanzia upya.
  • 7:14 - 7:20
    Sikufahamu wakati huohuo mambo yakawa kufukuzwa kwangu Apple kulinifanyia mema kwa kiwango cha juu.
  • 7:20 - 7:27
    Uzito ulionitwisha wa kufaulu kwangu ulichukuliwa na urahisi wa kuwepo mwanzoni kwa mara nyingine, nikiwaza na kuwazua.
  • 7:28 - 7:30
    Niliachiliwa huru kuanzisha muda wa ubunaji ulionufaika zaidi katika maisha yangu yote.
  • 7:31 - 7:35
    Katika miaka mitano iliyofuata nilianzisha kampuni jina lake, NeXT, nyingine jina lake Pixar,
  • 7:36 - 7:39
    nikampenda kwa dhati mwanamke wa aina yake akawa mke wangu.
  • 7:39 - 7:48
    Kampuni Pixar ikabunia sinema ya tarakilishi ya katuni hai ya kwanza katika dunia iitwao Toy Story halafu sasa Pixar imefaulu kushinda kampuni za katuni hai zote katika dunia.
  • 7:48 - 7:49
    [upigaji makofi na ukelele wa kufurahia]
  • 7:49 - 7:55
    Katika mabadiliko hayo ya matukio yasiyo na kifani, kampuni ya Apple ilinunua kampuni ya NeXT nami nikarudia Apple,
  • 7:55 - 7:59
    huku teknolojia iliyoundwa kampuni ya NeXT ikawa chimbuko la mvuvumko wa Apple wa leo hii.
  • 7:59 - 8:03
    Isitoshe mimi pamoja na mke wangu tumebarikiwa na familia nzuri mno.
  • 8:03 - 8:07
    Nina hakika mambo hayo yote hakungalifanikiwa endapo mimi nisipongelifukuzwa kazi Apple.
  • 8:08 - 8:11
    Ilikuwa dawa chungu kabisa lakini nakisia mimi nikiwa mgonjwa niliihitaji.
  • 8:12 - 8:16
    Wakati mwingine unapigwa kichwani na maisha.
  • 8:16 - 8:21
    Usipoteze imani. Mimi ninaamini ndio upendo wa kazi yangu ulionisukuma niendelee nayo.
  • 8:22 - 8:27
    Huna budi kutafuta lile unayolipenda ama ni kazi au wapenzi wako.
  • 8:28 - 8:34
    Kazi yako hula sehemu kubwa sana ya maisha yako, njia pekee kuridhika nayo ni kufanya ile unayoamini ni kazi muhimu mno.
  • 8:35 - 8:38
    Pia njia ya pekee katika kufanya kazi muhimu mno ni kupenda unayoifanya.
  • 8:39 - 8:43
    Endapo bado hujaikuta, endelea kuitafuta usikubali kwa shingo upande.
  • 8:43 - 8:47
    Kama yalivyo katika mambo ya mapenzi, utafahamu ndipo utakapoikuta.
  • 8:47 - 8:52
    Na kama yalivyo katika uhusiano wa kimapenzi kila ukipita wakati, nao unaendelea kuboreka.
  • 8:52 - 8:54
    Kwa hivyo endelea kuitafuta usikubali kwa shingo upande.
  • 8:57 - 9:04
    [Upigaji makofi]
  • 9:05 - 9:08
    Kisa changu cha tatu ni juu ya kifo.
  • 9:09 - 9:12
    Nilipokuwa na umri wa miaka kumi na saba nilisoma kidondoa kilichoeleweka kama:
  • 9:13 - 9:18
    "Ukiishia kila siku kama ni siku yako ya mwisho, siku moja ndipo itakuwepo."
  • 9:18 - 9:20
    [vichekesho]
  • 9:20 - 9:28
    Kidonda hicho kiliniathiri sana na tangu siku hiyo na kuendelea kwa muda wa miaka thelathini na mitatu, nimekuwa ninajitazama kwenye kioo nikijiuliza:
  • 9:28 - 9:33
    "Ikiwa leo ni siku ya mwisho maishani mwangu, ningefanya kama nimeshapanga nifanye leo hii?"
  • 9:33 - 9:39
    Wakati wowote jibu likiwa "hapana" kwa siku nyingi zaidi mfululizo, najua sina budi kubadilisha kitu fulani.
  • 9:40 - 9:47
    Nikikumbuka karibu nitakuwa nimeshakufa, ni kifaa muhimu kuliko vifaa vyote vingine nimekuwa navyo katika kunisaidia kufanya uchaguzi mkubwa katika maisha.
  • 9:47 - 9:54
    Kwa sababu karibu vitu vyote vinavyotarajiwa kutoka katika dunia, heshima zote, woga zote zu kutiliwa aibu au kushindwa
  • 9:54 - 10:00
    mambo hayo hutoweka yakiwa ana kwa ana na kifo, yanayobaki ni yale yenye umuhimu wa kweli.
  • 10:00 - 10:07
    Ukikumbuka hilo utakufa pasi na wasiwasi ya kufikiri kitu adimu kimekupotea.
  • 10:07 - 10:12
    Umeshaonekana bayana mtupu. Hakuna sababu kutofuatilia moyo wako.
  • 10:13 - 10:17
    Muda wa mwaka mmoja hivi uliopita nilipimwa nina saratani.
  • 10:18 - 10:23
    Nilipimwa mnamo saa moja u nusu asubuhi ikaonyesha bayana uvimbe wa kongosho.
  • 10:23 - 10:25
    Hata mimi sikujua kongosho ndicho kitu gani.
  • 10:26 - 10:35
    Madaktari walinieleza bila shaka saratani ya aina hii haina tibu ninatarajiwa kuishi muda usiozidi miezi mitatu hadi sita.
  • 10:35 - 10:43
    Daktari yangu alinishauri kwenda nyumbani nipange mambo yangu muhimu. Ndiyo mawaidha ya daktari kifo kinakuja.
  • 10:43 - 10:51
    Ndio maana kuwashauri watoto wako yote ya busara kawaida ungewaeleza katika muda wa miaka kumi sasa muda ndio miezi michache.
  • 10:51 - 10:56
    Ina maana kupanga utaratibu wa mambo yote ilimradi umewaepusha familia na matatizo na shida.
  • 10:57 - 10:59
    Ina maana ya kuwaaga wote wapendwa.
  • 11:01 - 11:03
    Nilikaa na utambuaji huo siku nzima.
  • 11:03 - 11:10
    Baadaye jioni ya siku hiyo nilipata uchunguzi wa tishu iliyokatwa kutoka katika uvimbe wa kongosho kwa kutumia endoscopu iliyopitishwa kwenye koo, kupitia tumbo hadi utumbo.
  • 11:10 - 11:14
    Kongosho ilipigwa sindano na seli chache zilivutwa kutoka katika uvimbe.
  • 11:15 - 11:23
    Mimi nilitulizwa na dawa lakini mke wangu naye alikuwepo akaniambia madaktari walipotazama seli kwa kutumia hadobini wakaanza kulia machozi,
  • 11:23 - 11:28
    kwa sababu ikagunduliwa aina ya saratani iliyoniumiza ni adimu sana na tibu inawezekana kutokana na upasuaji.
  • 11:28 - 11:32
    Nilipata upasuaji nashukuru Mungu sasa nimeshapoa.
  • 11:32 - 11:40
    [upigaji makofi]
  • 11:40 - 11:46
    Mara hiyo ndiyo ilinikaribisha na kifo zaidi. Nami matumaini ni hakitanikaribia tena kwa muda mrefu sana.
  • 11:46 - 11:54
    Kwa sababu nimeivumilia naweza kutamka kwa dhati zaidi kuliko wakati kifo kilikuwa wazo linalotumika bali likiwa dhana tupu.
  • 11:55 - 12:01
    Hakuna mtu anayetaka kufa. Hata wale wanayo hamu kwenda mbinguni hawataki kufa ili wapafike.
  • 12:01 - 12:07
    Hata hivyo kifo ni mwisho wa safari ya maisha tuliyonayo sisi sote. Hakuna mtu aliyejiepusha nacho.
  • 12:07 - 12:14
    Ndivyo yalivyo yawe yafaa kwani kifo kimebuniwa bora kuliko vitu vyote vingine maishani.
  • 12:14 - 12:18
    Ni kifaa kinachobadilisha maisha. Kinafutilia mbali yale yaliyokwisha zeeka huku kikikaribisha yale mapya.
  • 12:19 - 12:27
    Sasa yale mapya ndiyo ya nyinyi ingawaje siku moja si muda mrefu kutoka leo katika mwendo wa polepole mtakuwa waliozeeka mtafutiliwa mbali.
  • 12:27 - 12:31
    Naomba radhi nimetia chumvi lakini nimesema kweli.
  • 12:32 - 12:37
    Muda wenu una mwisho wake msije kuupoteza katika kuishi maisha ya mtu mwingine.
  • 12:37 - 12:42
    Usinaswe na porojo ambayo mfumo wake ni kuishi ukiwa na matokeo ya dhana za watu wengine.
  • 12:42 - 12:46
    Usiruhusu makelele ya maoni ya watu wengine kumeza sauti yako inayotokea moyoni mwako.
  • 12:46 - 12:50
    Na iliyo muhimu zaidi, uwe na ujasiri kufuatilia moyo wako welekevu wako.
  • 12:51 - 12:55
    Hisia hizo zimeshafahamu ukamilifu wa njia yako ya kimaisha.
  • 12:55 - 12:58
    mambo yote mengine hushika kiwango cha pili katika maisha.
  • 12:59 - 13:09
    [upigaji makofi]
  • 13:09 - 13:17
    Nilipokuwa kijana palikuwa na jarida la maajabu liitwalo "The Whoe Earth Catalog", ambalo lilikuwa kitabu muhimu mno kwa kizazi changu.
  • 13:17 - 13:25
    Kilibuniwa na mtu jina lake Stewart Brand aliyefanya kazi hiyo karibu kiasi na chuo hiki, naye alikijaza maana akiwa na kipaji cha utungaji mashairi.
  • 13:25 - 13:34
    Enzi hizo za sitini kabla ya tarakilishi ya kibinafsi na uchapishaji ofisini kwa hivyo lilitengenezwa na mashine ya chapa, mikasi, na kamera za kutoa picha mara moja.
  • 13:34 - 13:44
    Lilikuwa kama Google katika maumbile ya kitabu chenye jalada la karatasi muda wa miaka thelathini na tano kabla ya kuibuka kwa Google: Lilikuwa na maadili likimiminika na vifaa na madokezo mazuri sana.
  • 13:45 - 13:48
    Stewart akiwa na timu yake walitoa matoleo machache ya Whole Earth Catalog,
  • 13:48 - 13:52
    hatimaye lilipokaribu kwisha walitoa toleo la mwisho.
  • 13:52 - 13:56
    Wakati ulikuwa katikati ya enzi za sabini nami umri wangu sawa na wa nyinyi.
  • 13:58 - 14:07
    Juu ya jalada la mwisho ilikuwa foto ya njia sehemu za mashamba majira ya asubuhi ambako kuomba kuchukuliwa na gari hawatishi wasio na wasiwasi.
  • 14:08 - 14:16
    Chini ya foto palikuwa na maneno: "Endeleza njaa ya elimu." Ndio ujumbe wao wa mwisho wakitilia nanga uchapishaji. wa "Whole Earth Catalog".
  • 14:16 - 14:22
    Endeleza njaa ya elimu. Nami nimejiombea maneno hayo mwenyewe.
  • 14:23 - 14:28
    Sasa hivi mkihitimu tayari kuanzia upya, nawatakieni nyinyi maneno hayo.
  • 14:28 - 14:31
    Endeleza njaa ya elimu.
  • 14:31 - 14:32
    Asanteni sana
  • 14:33 - 14:49
    [upigaji makofi]
  • 14:54 - 14:57
    [Chuo Kikuu cha Stanford - www.stanford.edu]
  • 14:57 - 15:00
    Mtanganzaji: Kipindi hicho kimeidhiniwa na Chuo Kikuu cha Stanford.
  • 15:00 - 15:03
    Karibuni! Wasiliana nasi kwa stanford.edu
Title:
Hotuba ya Steve Jobs kwenye Sherehe ya Mahafali, Chuo Kikuu cha Stanford Mwaka wa 2005
Description:

Hii ni hotuba nyeti yenye mengi ya busara hasa kwa wanafunzi wa chuo kikuu wanaokabiliwa na uchaguzi wa masomo hatimaye ajira au ujasiriamali.

more » « less
Video Language:
English
Team:
Captions Requested
Duration:
15:05

Swahili subtitles

Revisions