WEBVTT 00:00:06.485 --> 00:00:07.508 [Chuo Kikuu cha Stanford www.stanford.edu] 00:00:07.508 --> 00:00:13.316 Mtangazaji: Kipindi hiki kimewaletea na Chuo Kikuu cha Stanford. Tafadhali wasiliana nasi kwa stanford.edu 00:00:15.055 --> 00:00:21.534 [upigaji makofi] 00:00:21.534 --> 00:00:22.842 Steve Jobs: Asanteni 00:00:24.964 --> 00:00:26.818 [Steve Jobs - Mkurugenzi Mkuu Apple na Pixar Animation] 00:00:27.034 --> 00:00:32.130 Ni heshima kwangu kuwepo na nyinyi katika sherehe ya mahafali ya kutunuku shahada kutoka katika chuo kikuu ambacho ni kimojawapo bora katika dunia nzima. 00:00:32.130 --> 00:00:35.381 [ukelele wa kufurahia] 00:00:35.689 --> 00:00:45.574 Kusema kweli mimi sijatunukiwa shahada ya chuo kikuu na hii ni mara yangu ya kwanza kuhudhuria mahafali yoyote. 00:00:46.098 --> 00:00:47.686 [vicheko] 00:00:47.948 --> 00:00:54.267 Leo naomba niwasimulie visa vitatu vilivyotokea maishani mwangu. Vitatu tu, basi. 00:00:55.481 --> 00:00:59.036 Cha kwanza ni juu ya kuunganisha nukta. 00:01:00.712 --> 00:01:08.197 Niliacha masomo katika Chuo cha Reed baada ya muda wa miezi sita za kwanza katika mwaka wa kwanza, halafu nikakaa kama mgeni kwa muda wa miezi kumi na nane hivi kabla ya kusimamisha masomo kabisa. 00:01:09.095 --> 00:01:10.834 Kwa nini niliacha masomo? 00:01:12.180 --> 00:01:13.949 Sababu inatangulia kuzaliwa kwangu. 00:01:15.101 --> 00:01:21.273 Mama mzazi yangu alikuwa msichana hajaolewa alikuwa akitimiza shahada ya uzamili akaamua niwe mtoto wa kupanga. 00:01:22.095 --> 00:01:25.988 Alikuwa na msimamo wa dhati nilelewe na watu waliotimiza shahada ya chuo kikuu. 00:01:25.988 --> 00:01:30.666 Kwa hivyo mpango ukafanyika niasiliwe na mwanasheria na mkewe. 00:01:31.581 --> 00:01:36.542 Isipokuwa nilipoibuka mtoto wa kiume dakika la mwisho wakaamua wanataka mtoto wa kike. 00:01:37.653 --> 00:01:42.346 Kwa hivyo wazazi wangu walioandikwa katika orodha ya wanaosubiri kumwasili mtoto walipigiwa simu usiku wa manane na wakaulizwa: 00:01:43.190 --> 00:01:49.204 "Tumepata mtoto wa kiume asiyetarajiwa; mnamtaka?" Wakajibu: "Bila shaka." 00:01:50.627 --> 00:01:58.247 Baadaye mama mzazi yangu aligundua mama yangu alikuwa hajamaliza chuo kikuu huku mumewe baba yangu hajamaliza shule ya sekondari. 00:01:58.775 --> 00:02:02.116 Akakataa kutia sahihi hati maalum ya kuasiliwa. 00:02:03.275 --> 00:02:11.678 Baada ya miezi michache kupita akakubali shingo upande kutokana na ahadi ya wazazi wapya ya kuwa mimi nitasoma chuo kikuu. Hayo ndiyo yalikuwa mwanzo wa maisha yangu. 00:02:13.649 --> 00:02:21.452 Baada ya miaka kumi na saba kupita nilianza chuo kikuu lakini katika ushamba wangu nikachagua chuo ghali karibu sawa na Stanford. 00:02:22.207 --> 00:02:26.584 Pesa zote za akiba ya wazazi wangu tabaka yao ya wafanya kazi, zilitumika kulipia ada zangu za chuo kikuu. 00:02:27.303 --> 00:02:30.175 Baada ya muda wa miezi sita sikuona thamani ya masomo hayo. 00:02:30.458 --> 00:02:35.932 Sikuwa na mpango wa maisha mbali na uwezo wa chuo kunisaidia katika kufafanua mpango upi unanifaa zaidi. 00:02:36.582 --> 00:02:40.850 Huku nikitumia pesa zote za akiba ya maisha ya wazazi wangu. 00:02:42.323 --> 00:02:46.790 Basi nikakata shauri kuachana na masomo nikiamini mambo yatakuwa shwari. 00:02:47.408 --> 00:02:52.249 Wasiwasi ilinikumba wakati huohuo lakini sasa nikilitafakari shauri hilo ni miongoni mwa yale bora katika maisha yangu. 00:02:52.937 --> 00:02:53.991 [vicheko] 00:02:54.068 --> 00:02:59.071 Pindi tu nilipoachana sikulazimishwa kuchukua madarasa yale ambayo hayakunivutia. 00:02:59.501 --> 00:03:03.504 Nikaenda kwa yale yaliyovutia kwangu. 00:03:04.580 --> 00:03:13.822 Sikuwa na maisha ya starehe. Sikuwa na chumba katika bweni. Ilibidi nilale sakafuni katika vyumba vya marafiki. Nilikuwa nikiokota chupa kupata senti za kununulia chakula. 00:03:14.397 --> 00:03:21.312 Kila Jumapili mimi hutembeza maili saba ili nipata lishe maalum katika hekalu ya Wahindi wafuasi wa dini ya Hare Krishna. 00:03:21.716 --> 00:03:23.210 Niliipenda mno. 00:03:23.580 --> 00:03:29.722 Mengi niliyowahi kutokana na upekuzi wangu pamoja na uwezo wangu kuelewa yakawa adimu nyakati za baadaye. 00:03:29.876 --> 00:03:31.354 Hebu, nitoe mfano mmoja: 00:03:32.759 --> 00:03:37.683 Wakati huo Chuo cha Reed kilikuwa na ufundisho bora wa utaalamu wa maandiko kuliko vyuo vyote vingine nchini. 00:03:37.992 --> 00:03:44.635 Kwenye eneo la chuo kila tangazo, kila kitambulisho kwenye mitoto ya meza kilichorwa vizuri sana. 00:03:45.024 --> 00:03:52.489 Kwa sababu nimeshajitoa masomoni sikulazimishwa kuchukua madarasa yanayotakiwa na nikaamua kuchukua darasa la utaalamu wa maandiko nijifunze jinsi ya kufanya. 00:03:52.692 --> 00:03:59.285 Nilijifunza aina za chapa mifano ni serif na sans serif, juu ya upimaji nafasi katikati ya michanganyiko tofauti ya herufi, 00:03:59.582 --> 00:04:02.355 na juu ya ukamilifu wa utaalamu wa maandiko, kitu gani kinaleta ukamilifu. 00:04:02.899 --> 00:04:11.026 Kujifunza huko kulikuwa kuzuri, kwenye usanaa usio na kujivuna mbali na mazingira ya kisayansi, kwangu mimi nilivutiwa kupindukia. 00:04:11.730 --> 00:04:16.231 Sikuwa na matumaini ya kuyatumia masomo hayo katika kazi nitakayofanya, 00:04:17.005 --> 00:04:22.911 Lakini baada ya muda wa miaka kumi kupita tulipokuwa tunabunia tarakilishi ya kwanza aina ya Mactintosh nikafikiria upya mafundisho hayo. 00:04:23.050 --> 00:04:28.612 Tulitumia kabisa katika ubunaji wa Mac ambayo ilikuwa tarakilishi ya kwanza kuwa na utaalamu mzuri wa maandiko. 00:04:29.077 --> 00:04:32.364 Nisingeli kuwa mgeni katika darasa hilo nilipokuwa ninahangaika kwenye chuo, 00:04:32.486 --> 00:04:36.549 tarakilishi iitwayo Mac haikungali kuwa na aina nyingi za herufi wala herufi zenye uwiano wa nafasi za katikati zao. 00:04:36.962 --> 00:04:42.231 Na kwa sababu Windows iliiga Mac haielekei tarakilishi za kibinafisi zozote zingekuwa nazo kamwe. 00:04:42.468 --> 00:04:49.387 [vicheko na upigaji makofi] 00:04:49.572 --> 00:04:53.668 Nisipongeliachana na masomo singalipitia darasa lile la utaalamu wa maandiko. 00:04:53.729 --> 00:04:57.601 matokeo yake tarakilishi ya kibinafsi hazingekuwa na vivutio kiasi zinazokuwa nazo. 00:04:57.923 --> 00:05:02.194 Bila shaka ilikuwa haiwezekani kuunganisha nukta zitakazokuja mambo ya usoni nilipokuwa chuoni. 00:05:02.484 --> 00:05:06.349 Lakini mambo yakadhihirika kweupe nikirudia nyuma baada ya muda wa miaka kumi kupita. 00:05:06.595 --> 00:05:12.104 Kutia mkazo kauli hiyo, huwezi kuunganisha nukta za mambo ya usoni; ni zile tu zilizokwisha fanyika ambazo zinaweza kuzingatiwa ziunganishwe, 00:05:12.374 --> 00:05:16.162 Lazima uamini nukta za baadaye zitaunganika katika maisha yako ya baadaye. 00:05:16.365 --> 00:05:21.131 Sharti uwe na uaminifu wa huenda moyo wako, majaliwa, maisha, hulka zako, na kadhalika. 00:05:21.374 --> 00:05:27.284 Kwa sababu kuamini nukta zitaunganika baadaye kutakutilia moyo na imani kupiga njia uliyoinyoshea wewe mwenyewe. 00:05:27.468 --> 00:05:32.111 Hata ukifuata njia isiyo ya kawaida, uaminifu ndio utakunyoshea. 00:05:37.972 --> 00:05:42.253 Kisa changu cha pili ni juu ya upendo na kukosa upendo. 00:05:43.408 --> 00:05:47.535 Mimi nilibahatika - nilipata kujua ninavyopenda kufanya nikiwa bado mvulana. 00:05:47.977 --> 00:05:51.156 Mimi pamoja na rafiki yangu jina lake Woz tulianzisha kampuni la Apple kwenye kibanda cha gari nyumbani kwao wazazi wangu na mimi nikiwa na umri wa miaka ishirini. 00:05:51.367 --> 00:05:59.303 Tulifanya kazi kwa bidii na baada ya muda wa miaka kumi kampuni ya Apple iliyoanzia na watu wawili sisi tukiwa kwenye kibanda, ilikua kupata thamani ya dola bilioni mbili ikiwa na waajiriwa zaidi ya elfu nne. 00:05:59.608 --> 00:06:04.777 Tulikuwa tumetoa maumbile yetu bora - Macintosh, mwaka mmoja kabla, nami nikipata umri wa miaka thelathini. 00:06:05.937 --> 00:06:07.168 Kisha nikafukuzwa kazini. 00:06:08.545 --> 00:06:11.115 Je, inawezaje kufukuzwa kutoka kampuni uliyoanzisha wewe mwenyewe? 00:06:11.913 --> 00:06:18.038 Basi kama kampuni ya Apple ilivyoendelea kukua tukaajiri mtu mwenye kipaji kizuri kuongoza kampuni akiwa na mimi, 00:06:18.254 --> 00:06:20.527 na mwaka wa kwanza mambo yakawa shwari. 00:06:20.681 --> 00:06:25.095 Halafu baada ya hapo mitazamo yetu ikaanza kutengana hatimaye tukafarakana. 00:06:25.258 --> 00:06:28.229 Tulipofarakana baraza letu la wakurugenzi wakamuunga mkono yeye. 00:06:28.447 --> 00:06:32.351 Kwa hivyo nikiwa na umri wa miaka thelathini nilifukuzwa kazi bayana ikatangazwa kwenye magazeti. 00:06:32.827 --> 00:06:37.441 Kitu kilichokuwa kitovu cha maisha yangu nikiwa mtu mzima kimekwisha, nami nikadhoofika. 00:06:37.857 --> 00:06:40.057 Kwa muda wa miezi michache, kweli nilikuwa sikujua la kufanya. 00:06:40.645 --> 00:06:46.997 Niliona nimewasikitisha wale wajasiriamali wa kizazi kilichotangulia - nikashindwa kubeba amali ilyonipasa niibebe. 00:06:47.589 --> 00:06:53.238 Tulikutana na David Packard pamoja na Bob Noyce nikaomba radhi kwa kuharibu mambo. 00:06:53.796 --> 00:06:57.664 Kushindwa kwangu kulijulikana na wengi hata nilifikiri kukimbia Bonde. 00:06:57.977 --> 00:07:03.285 Lakini katika mwendo polepole nilitanabahi ya kuwa bado niliipenda kazi yangu. 00:07:04.316 --> 00:07:10.651 Mambo yaleyale ya mabadiliko pale Apple hayajaubadilisha upendo wangu hata kidogo. 00:07:11.647 --> 00:07:13.309 Kwa hivyo basi nikaamua kuanzia upya. 00:07:14.345 --> 00:07:20.374 Sikufahamu wakati huohuo mambo yakawa kufukuzwa kwangu Apple kulinifanyia mema kwa kiwango cha juu. 00:07:20.482 --> 00:07:27.122 Uzito ulionitwisha wa kufaulu kwangu ulichukuliwa na urahisi wa kuwepo mwanzoni kwa mara nyingine, nikiwaza na kuwazua. 00:07:27.611 --> 00:07:30.442 Niliachiliwa huru kuanzisha muda wa ubunaji ulionufaika zaidi katika maisha yangu yote. 00:07:30.887 --> 00:07:35.481 Katika miaka mitano iliyofuata nilianzisha kampuni jina lake, NeXT, nyingine jina lake Pixar, 00:07:35.802 --> 00:07:38.633 nikampenda kwa dhati mwanamke wa aina yake akawa mke wangu. 00:07:38.931 --> 00:07:47.529 Kampuni Pixar ikabunia sinema ya tarakilishi ya katuni hai ya kwanza katika dunia iitwao Toy Story halafu sasa Pixar imefaulu kushinda kampuni za katuni hai zote katika dunia. 00:07:47.804 --> 00:07:49.443 [upigaji makofi na ukelele wa kufurahia] 00:07:49.443 --> 00:07:54.585 Katika mabadiliko hayo ya matukio yasiyo na kifani, kampuni ya Apple ilinunua kampuni ya NeXT nami nikarudia Apple, 00:07:54.764 --> 00:07:58.841 huku teknolojia iliyoundwa kampuni ya NeXT ikawa chimbuko la mvuvumko wa Apple wa leo hii. 00:07:59.261 --> 00:08:02.508 Isitoshe mimi pamoja na mke wangu tumebarikiwa na familia nzuri mno. 00:08:03.317 --> 00:08:07.131 Nina hakika mambo hayo yote hakungalifanikiwa endapo mimi nisipongelifukuzwa kazi Apple. 00:08:07.573 --> 00:08:11.147 Ilikuwa dawa chungu kabisa lakini nakisia mimi nikiwa mgonjwa niliihitaji. 00:08:11.740 --> 00:08:15.742 Wakati mwingine unapigwa kichwani na maisha. 00:08:15.971 --> 00:08:21.314 Usipoteze imani. Mimi ninaamini ndio upendo wa kazi yangu ulionisukuma niendelee nayo. 00:08:21.761 --> 00:08:26.982 Huna budi kutafuta lile unayolipenda ama ni kazi au wapenzi wako. 00:08:27.639 --> 00:08:34.280 Kazi yako hula sehemu kubwa sana ya maisha yako, njia pekee kuridhika nayo ni kufanya ile unayoamini ni kazi muhimu mno. 00:08:34.510 --> 00:08:38.331 Pia njia ya pekee katika kufanya kazi muhimu mno ni kupenda unayoifanya. 00:08:38.567 --> 00:08:42.651 Endapo bado hujaikuta, endelea kuitafuta usikubali kwa shingo upande. 00:08:43.067 --> 00:08:46.503 Kama yalivyo katika mambo ya mapenzi, utafahamu ndipo utakapoikuta. 00:08:46.694 --> 00:08:51.513 Na kama yalivyo katika uhusiano wa kimapenzi kila ukipita wakati, nao unaendelea kuboreka. 00:08:51.631 --> 00:08:54.280 Kwa hivyo endelea kuitafuta usikubali kwa shingo upande. 00:08:57.469 --> 00:09:04.165 [Upigaji makofi] 00:09:04.658 --> 00:09:07.612 Kisa changu cha tatu ni juu ya kifo. 00:09:08.730 --> 00:09:12.062 Nilipokuwa na umri wa miaka kumi na saba nilisoma kidondoa kilichoeleweka kama: 00:09:12.532 --> 00:09:17.716 "Ukiishia kila siku kama ni siku yako ya mwisho, siku moja ndipo itakuwepo." 00:09:18.030 --> 00:09:19.750 [vichekesho] 00:09:20.350 --> 00:09:27.501 Kidonda hicho kiliniathiri sana na tangu siku hiyo na kuendelea kwa muda wa miaka thelathini na mitatu, nimekuwa ninajitazama kwenye kioo nikijiuliza: 00:09:27.647 --> 00:09:33.201 "Ikiwa leo ni siku ya mwisho maishani mwangu, ningefanya kama nimeshapanga nifanye leo hii?" 00:09:33.383 --> 00:09:38.989 Wakati wowote jibu likiwa "hapana" kwa siku nyingi zaidi mfululizo, najua sina budi kubadilisha kitu fulani. 00:09:39.905 --> 00:09:46.643 Nikikumbuka karibu nitakuwa nimeshakufa, ni kifaa muhimu kuliko vifaa vyote vingine nimekuwa navyo katika kunisaidia kufanya uchaguzi mkubwa katika maisha. 00:09:47.254 --> 00:09:54.097 Kwa sababu karibu vitu vyote vinavyotarajiwa kutoka katika dunia, heshima zote, woga zote zu kutiliwa aibu au kushindwa 00:09:54.097 --> 00:09:59.842 mambo hayo hutoweka yakiwa ana kwa ana na kifo, yanayobaki ni yale yenye umuhimu wa kweli. 00:09:59.949 --> 00:10:07.279 Ukikumbuka hilo utakufa pasi na wasiwasi ya kufikiri kitu adimu kimekupotea. 00:10:07.462 --> 00:10:12.389 Umeshaonekana bayana mtupu. Hakuna sababu kutofuatilia moyo wako. 00:10:13.118 --> 00:10:16.660 Muda wa mwaka mmoja hivi uliopita nilipimwa nina saratani. 00:10:17.559 --> 00:10:22.533 Nilipimwa mnamo saa moja u nusu asubuhi ikaonyesha bayana uvimbe wa kongosho. 00:10:22.746 --> 00:10:25.038 Hata mimi sikujua kongosho ndicho kitu gani. 00:10:25.514 --> 00:10:34.658 Madaktari walinieleza bila shaka saratani ya aina hii haina tibu ninatarajiwa kuishi muda usiozidi miezi mitatu hadi sita. 00:10:34.927 --> 00:10:42.652 Daktari yangu alinishauri kwenda nyumbani nipange mambo yangu muhimu. Ndiyo mawaidha ya daktari kifo kinakuja. 00:10:42.944 --> 00:10:50.659 Ndio maana kuwashauri watoto wako yote ya busara kawaida ungewaeleza katika muda wa miaka kumi sasa muda ndio miezi michache. 00:10:51.149 --> 00:10:56.482 Ina maana kupanga utaratibu wa mambo yote ilimradi umewaepusha familia na matatizo na shida. 00:10:56.810 --> 00:10:58.642 Ina maana ya kuwaaga wote wapendwa. 00:11:00.514 --> 00:11:02.940 Nilikaa na utambuaji huo siku nzima. 00:11:03.389 --> 00:11:10.265 Baadaye jioni ya siku hiyo nilipata uchunguzi wa tishu iliyokatwa kutoka katika uvimbe wa kongosho kwa kutumia endoscopu iliyopitishwa kwenye koo, kupitia tumbo hadi utumbo. 00:11:10.452 --> 00:11:14.069 Kongosho ilipigwa sindano na seli chache zilivutwa kutoka katika uvimbe. 00:11:14.587 --> 00:11:22.526 Mimi nilitulizwa na dawa lakini mke wangu naye alikuwepo akaniambia madaktari walipotazama seli kwa kutumia hadobini wakaanza kulia machozi, 00:11:22.721 --> 00:11:27.711 kwa sababu ikagunduliwa aina ya saratani iliyoniumiza ni adimu sana na tibu inawezekana kutokana na upasuaji. 00:11:28.214 --> 00:11:31.835 Nilipata upasuaji nashukuru Mungu sasa nimeshapoa. 00:11:32.057 --> 00:11:39.699 [upigaji makofi] 00:11:40.142 --> 00:11:45.621 Mara hiyo ndiyo ilinikaribisha na kifo zaidi. Nami matumaini ni hakitanikaribia tena kwa muda mrefu sana. 00:11:45.960 --> 00:11:53.539 Kwa sababu nimeivumilia naweza kutamka kwa dhati zaidi kuliko wakati kifo kilikuwa wazo linalotumika bali likiwa dhana tupu. 00:11:54.797 --> 00:12:00.852 Hakuna mtu anayetaka kufa. Hata wale wanayo hamu kwenda mbinguni hawataki kufa ili wapafike. 00:12:01.324 --> 00:12:07.074 Hata hivyo kifo ni mwisho wa safari ya maisha tuliyonayo sisi sote. Hakuna mtu aliyejiepusha nacho. 00:12:07.351 --> 00:12:13.946 Ndivyo yalivyo yawe yafaa kwani kifo kimebuniwa bora kuliko vitu vyote vingine maishani. 00:12:14.116 --> 00:12:18.353 Ni kifaa kinachobadilisha maisha. Kinafutilia mbali yale yaliyokwisha zeeka huku kikikaribisha yale mapya. 00:12:18.910 --> 00:12:27.124 Sasa yale mapya ndiyo ya nyinyi ingawaje siku moja si muda mrefu kutoka leo katika mwendo wa polepole mtakuwa waliozeeka mtafutiliwa mbali. 00:12:27.463 --> 00:12:30.697 Naomba radhi nimetia chumvi lakini nimesema kweli. 00:12:31.777 --> 00:12:36.719 Muda wenu una mwisho wake msije kuupoteza katika kuishi maisha ya mtu mwingine. 00:12:37.099 --> 00:12:41.787 Usinaswe na porojo ambayo mfumo wake ni kuishi ukiwa na matokeo ya dhana za watu wengine. 00:12:42.272 --> 00:12:46.125 Usiruhusu makelele ya maoni ya watu wengine kumeza sauti yako inayotokea moyoni mwako. 00:12:46.333 --> 00:12:50.250 Na iliyo muhimu zaidi, uwe na ujasiri kufuatilia moyo wako welekevu wako. 00:12:50.763 --> 00:12:54.518 Hisia hizo zimeshafahamu ukamilifu wa njia yako ya kimaisha. 00:12:54.896 --> 00:12:57.539 mambo yote mengine hushika kiwango cha pili katika maisha. 00:12:59.280 --> 00:13:08.542 [upigaji makofi] 00:13:08.773 --> 00:13:17.200 Nilipokuwa kijana palikuwa na jarida la maajabu liitwalo "The Whoe Earth Catalog", ambalo lilikuwa kitabu muhimu mno kwa kizazi changu. 00:13:17.302 --> 00:13:24.767 Kilibuniwa na mtu jina lake Stewart Brand aliyefanya kazi hiyo karibu kiasi na chuo hiki, naye alikijaza maana akiwa na kipaji cha utungaji mashairi. 00:13:25.231 --> 00:13:33.542 Enzi hizo za sitini kabla ya tarakilishi ya kibinafsi na uchapishaji ofisini kwa hivyo lilitengenezwa na mashine ya chapa, mikasi, na kamera za kutoa picha mara moja. 00:13:33.765 --> 00:13:44.032 Lilikuwa kama Google katika maumbile ya kitabu chenye jalada la karatasi muda wa miaka thelathini na tano kabla ya kuibuka kwa Google: Lilikuwa na maadili likimiminika na vifaa na madokezo mazuri sana. 00:13:44.550 --> 00:13:47.915 Stewart akiwa na timu yake walitoa matoleo machache ya Whole Earth Catalog, 00:13:48.202 --> 00:13:52.173 hatimaye lilipokaribu kwisha walitoa toleo la mwisho. 00:13:52.496 --> 00:13:56.349 Wakati ulikuwa katikati ya enzi za sabini nami umri wangu sawa na wa nyinyi. 00:13:57.529 --> 00:14:07.291 Juu ya jalada la mwisho ilikuwa foto ya njia sehemu za mashamba majira ya asubuhi ambako kuomba kuchukuliwa na gari hawatishi wasio na wasiwasi. 00:14:07.912 --> 00:14:15.784 Chini ya foto palikuwa na maneno: "Endeleza njaa ya elimu." Ndio ujumbe wao wa mwisho wakitilia nanga uchapishaji. wa "Whole Earth Catalog". 00:14:16.275 --> 00:14:22.072 Endeleza njaa ya elimu. Nami nimejiombea maneno hayo mwenyewe. 00:14:22.758 --> 00:14:27.763 Sasa hivi mkihitimu tayari kuanzia upya, nawatakieni nyinyi maneno hayo. 00:14:28.012 --> 00:14:30.602 Endeleza njaa ya elimu. 00:14:30.905 --> 00:14:32.382 Asanteni sana 00:14:32.591 --> 00:14:49.110 [upigaji makofi] 00:14:54.314 --> 00:14:56.841 [Chuo Kikuu cha Stanford - www.stanford.edu] 00:14:56.918 --> 00:15:00.210 Mtanganzaji: Kipindi hicho kimeidhiniwa na Chuo Kikuu cha Stanford. 00:15:00.357 --> 00:15:03.147 Karibuni! Wasiliana nasi kwa stanford.edu