Return to Video

Out of Poverty: Paul Polak on Practical Problem Solving

  • 0:06 - 0:10
    Baada ya kuwafanyia usahili maelfu ya wakulima masikini
  • 0:10 - 0:17
    katika nchi kama Nepal, Bangladesh, China, Mexico, na Zambia
  • 0:17 - 0:21
    Nimejifunza kwamba utatuzi wa kivitendo katika umasikini uliokithiri
  • 0:21 - 0:25
    unaweza kupatikana kwa kuwasikiliza watu hao masikini
  • 0:25 - 0:30
    na sio toka kwa jeshi la wataalam wa umasikini duniani.
  • 0:30 - 0:34
    Nimetengeneza hatua 12 za kivitendo kwa ajili ya utatuzi wa matatizo
  • 0:34 - 0:38
    ambazo zimesaidia watu 17 milioni kuondokana na umasikini
  • 0:38 - 0:42
    na kuwepo katika tabaka la kati milele.
  • 0:42 - 0:47
    Hatua hizi 12 zinatumika vizuri pia katika kutafuta hatua za kivitendo za utatuzi
  • 0:47 - 0:51
    katika matatizo makubwa ya kijamii ambayo unaweza ukawa unayafanyia kazi.
  • 0:51 - 0:57
    Nimezielezea hatua hizi 12 katika kitabu changu cha, Out of Poverty.
  • 0:57 - 0:59
    Kwa miaka mitano iliyopita nimekuwa nikifanyia kazi kitabu
  • 0:59 - 1:02
    na hatimaye nimekimaliza.
  • 1:02 - 1:07
    Imenichukua miaka mitano kuandika kurasa 200 tu.
  • 1:07 - 1:11
    Kitabu kinaitwa Out of Poverty:
  • 1:11 - 1:17
    What works when traditional approaches fail.
  • 1:17 - 1:21
    Kwa kweli nimeandika kitabu hicho kuleta mapinduzi
  • 1:21 - 1:26
    katika tunavyofikiri juu ya umasikini na yale tunayofanya juu yake.
  • 1:26 - 1:32
    Hakitaweza kuleta mapinduzi chenyewe lakini nina imani kitasaidia.
  • 1:32 - 1:39
    Kwa miaka 25 iliyopita maswali mawili yamegandama udadisi wangu.
  • 1:39 - 1:42
    Nini kinawafanya watu masikini kuwa masikini?
  • 1:42 - 1:47
    Na kitu gani wanaweza kufanya juu ya hali hiyo?
  • 1:47 - 1:51
    Kwa sababu ya maswali haya mawili yanayokera,
  • 1:51 - 1:58
    Nimekuwa na mazungumzo marefu na wamiliki maelfu wa eka moja katika nchi zinazoendelea.
  • 1:58 - 2:02
    Nilichojifunza kimeleta uwezekano kwa IDE,
  • 2:02 - 2:05
    asasi ya kimaendeleo niliyoianzisha miaka 25 iliyopita,
  • 2:05 - 2:13
    kusaidia watu 17 milioni watu wa $1-kwa-siku kuondokana na umasikini milele.
  • 2:13 - 2:17
    Hatua tatu za kwanza za utatuzi wa kivitendo wa matatizo ni
  • 2:17 - 2:23
    yawezekana zilizo wazi zaidi, zilizo rahisi zaidi, na zinazofuatwa kwa kiwango kidogo zaidi.
  • 2:23 - 2:29
    Ya kwanza ni kwenda pale tendo liliko.
  • 2:29 - 2:31
    Uwezi ukakaa katika ofisi yako katika Benki ya Dunia
  • 2:31 - 2:38
    na ukagundua jinsi ya kutatua matatizo ya umasikini Myanmar.
  • 2:38 - 2:41
    Hatua ya 2, ongea na watu ambao wana hilo tatizo
  • 2:41 - 2:45
    na sikiliza yale watakayosema.
  • 2:45 - 2:51
    Katika miaka ya 1990, wataalam wa kilimo wa Bangladesh walisikitishwa
  • 2:51 - 2:58
    na viwango finyu vya mbolea wakulima wa Bangladesh walivyotumia katika mazao yao ya mchele/mpunga (monsoon rice crops).
  • 2:58 - 3:03
    Wakaanzisha programu za mafunzo kwa wakulima lakini hakuna kilichofanya kazi.
  • 3:03 - 3:08
    Hatimaye, mtu mmoja akawauliza baadhi ya wakulima kwanini wanatumia kiwango kidogo sana cha mbolea.
  • 3:08 - 3:10
    “Hilo rahisi,” walisema.
  • 3:10 - 3:15
    “Kila baada ya miaka 10 hivi tunakuwa na mafuriko makubwa yanayosafisha kila kitu tulichopanda. ..."
  • 3:15 - 3:22
    "... Kwa hiyo tunatumia kiwango sawia cha mbolea tunachoweza kumudu katika mafuriko ya miaka 10.”
  • 3:22 - 3:30
    Punde wakulima hawa wakabadilishwa toka katika ujinga, woga,
  • 3:30 - 3:35
    na kuwa watu wanaoweza kuwafundisha wataalam wa kilimo kitu fulani.
  • 3:35 - 3:41
    Hatua ya 3, jifunze kila kitu kilichopo juu ya mazingira na hali halisi ya tatizo husika.
  • 3:41 - 3:44
    Mazingira halisi ya watu 800 milioni
  • 3:44 - 3:48
    kati ya watu 1.2 bilioni duniani wanaoishi kwa chini ya $2 kwa siku,
  • 3:48 - 3:55
    ni kashamba kadogo chenye udongo usio na rutuba na hakuna umwagiliaji.
  • 3:55 - 3:57
    Mashamba haya sanasana ni ya eka moja,
  • 3:57 - 4:02
    na yamegawanywa katika ploti 4 au 5.
  • 4:02 - 4:03
    Na hili ni wazo la nne,
  • 4:03 - 4:09
    kama utagundua utatuzi juu ya tatizo hakuna sababu ya kuwa wastani.
  • 4:09 - 4:14
    Baadhi ya matatizo makubwa sana duniani katika hali halisi yanahitaji utatuzi madhubuti/mkubwa
  • 4:14 - 4:21
    ambao katika hali halisi ni utatuzi mdogomdogo unaotekelezwa mara maelfu na maelfu.
  • 4:21 - 4:24
    Hatua ya 5, fikiri kama mtoto.
  • 4:24 - 4:31
    Inakinzana kidogo kwamba kufikiri makubwa na kufikiri kama mtoto vinaenda pamoja, lakini inakuwa hivyo.
  • 4:31 - 4:38
    Inabidi ufikiri kama mtoto ili kupata utatuzi ulio wazi juu ya tatizo kubwa ambalo watu wamelishindwa.
  • 4:38 - 4:43
    Hatua ya 6, angalia na fanya kilicho wazi.
  • 4:43 - 4:48
    Kama hatuwezi kuona upofu wetu ni vipi tutaona na kufanya kilicho wazi?
  • 4:48 - 4:53
    Kujiweka katika tatizo kunasaidia.
  • 4:53 - 4:58
    Hatua ya 7, kama tayari kuna mtu amekwisha buni hauhitajiki kufanya hivyo.
  • 4:58 - 5:05
    Ni rahisi siku hizi kufuatilia utatuzi ambao tayari watu wameshautoa.
  • 5:05 - 5:15
    Hatua ya 8, hakikisha mkabala wako una matokeo chanya yanayopimika na yanayoweza kukuzwa/kuwekwa katika skeli.
  • 5:15 - 5:21
    Hatua ya 9, sanifu ukilenga bei fulani.
  • 5:21 - 5:27
    Kumudu bei kunatawala mchakato wa usanifu kwa wateja masikini.
  • 5:27 - 5:31
    Namba 10, fuata mipango ya kivitendo ya miaka 3.
  • 5:31 - 5:36
    Bila kujali kiwango cha nguvu na ubadilishaji wa dunia katika dira yako juu ya mambo ya mbele,
  • 5:36 - 5:42
    kama hautaweza kutafsiri katika mpango madhubuti ndani ya miaka mitatu ya mwanzo,
  • 5:42 - 5:46
    hautaweza kufikia lengo.
  • 5:46 - 5:52
    Hatua ya 11, endelea kujifunza toka kwa wateja wako.
  • 5:52 - 5:58
    Nilipoanzisha IDE niliamua kwamba nitahudumu angalau wateja 100 kwa mwaka
  • 5:58 - 6:00
    na nimefanya hivyo.
  • 6:00 - 6:07
    Mpaka sasa nimehoji zaidi ya familia masikini za wakulima 3000,
  • 6:07 - 6:12
    na nimetembea nao katika mashamba yao.
  • 6:12 - 6:15
    Waliponiambia kwamba wamewekeza
  • 6:15 - 6:16
    vipato vyao vipya toka kwenye treadle pump
  • 6:16 - 6:19
    kwenye elimu ya watoto wao,
  • 6:19 - 6:22
    tulisanifu taa ya umeme jua ya $12
  • 6:22 - 6:26
    ili watoto wao waweze kusoma usiku.
  • 6:26 - 6:27
    Waliposema wamewekeza
  • 6:27 - 6:30
    sehemu ya fedha zao toka kwenye mifumo ya umwagiliaji ya dripu
  • 6:30 - 6:34
    katika nyati wa maziwa ama katika idadi ya mbuzi,
  • 6:34 - 6:37
    tulijifunza kila kitu kilichohitajika juu ya ufugaji mdogo
  • 6:37 - 6:44
    na tukaanza kusaidia wakulima walio na miradi midogo ya ufugaji.
  • 6:44 - 6:49
    Namba 12, usiyumbishwe na yale yanayosemwa na watu wengine.
  • 6:49 - 6:52
    Katika kila kitu ambacho nimefanyia kazi
  • 6:52 - 6:55
    na kugeuka kuwa mafanikio makubwa,
  • 6:55 - 7:00
    Nimesikia watu wengi wakiniambia kwamba napoteza muda.
  • 7:00 - 7:03
    Milioni moja na nusu ya treadle pumps baadae,
  • 7:03 - 7:10
    tuna ekari mpya elfu 750 chini ya umwagiliaji.
  • 7:10 - 7:14
    Kama ningewasikiliza watu waliosema ni kupoteza muda,
  • 7:14 - 7:17
    tusingefika hapo.
  • 7:17 - 7:20
    Kama una nia ya kuwa sehemu ya kitu haswa,
  • 7:20 - 7:25
    tembelea watu katika mazingira yao halisi
  • 7:25 - 7:30
    na sikiliza wanachosema,
  • 7:30 - 7:31
    na muhimu sana,
  • 7:31 - 7:34
    kuwa na nia ya kujifunza mambo mapya,
  • 7:34 - 7:36
    hapo mkabala huu utakuwa kwa ajili yako.
  • 7:36 - 7:39
    Kama wewe na kundi lako mtaamua kwamba kitu bora mtakachofanya nia kutoa msaada wa fedha,
  • 7:39 - 7:43
    hakikisha unachagua asasi zilizo na matokeo yanayopimika,
  • 7:43 - 7:47
    kama asasi za umasikini zinazoongeza kipato
  • 7:47 - 8:25
    cha watu wanaoishi kwa chini ya dola moja kwa siku.
Title:
Out of Poverty: Paul Polak on Practical Problem Solving
Description:

Paul Polak, author of Out of Poverty: What Works When Traditional Approaches Fail, discusses his 12 steps for effective problem solving to end global poverty.

more » « less
Video Language:
English
Duration:
08:39
LucasG added a translation

Swahili subtitles

Revisions